Ezekiel 18:5-10


5 “Mtu aweza kuwa ni mwenye haki
atendaye yaliyo haki na sawa.

6 aHakula katika mahali pa ibada za miungu
kwenye milima
wala hakuziinulia macho sanamu
za nyumba ya Israeli.
Hakumtia unajisi mke wa jirani yake,
wala hakukutana kimwili na mwanamke
wakati wa siku zake za hedhi.

7 bHamwonei mtu yeyote,
bali hurudisha kilichowekwa rehani kwake.
Hanyang’anyi, bali huwapa wenye njaa chakula chake
na huwapa nguo walio uchi.

8 cHakopeshi kwa riba
wala hajipatii faida ya ziada.
Huuzuia mkono wake usifanye mabaya,
naye huhukumu kwa haki kati ya mtu na mtu.

9 dHuzifuata amri zangu
na kuzishika sheria zangu kwa uaminifu.
Huyo mtu ni mwenye haki;
hakika ataishi,
asema Bwana Mwenyezi.

10 e“Aweza kuwa ana mwana jeuri, amwagaye damu au atendaye mojawapo ya mambo haya
Copyright information for SwhKC